BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, August 31, 2010

NASSIR A.K.A 'OBAMA' KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM KOROGWE!

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, kushoto akiwa na mwenyekiti wa CCM Mkowa wa Tanga Mussa Shekimweli kulia wakati wakiwapungia wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la Korogwe mji iliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mazoezi.

MWANAFUNZI wa Naibu waziri wa wizara ya habari na utamaduni Joel Bendera amepata ridhaa ya kupambana katika kinyang'anyiro cha ubunge kupitia CCM wilayani Korogwe. Nassir almaarufu "Obama" ndiye aliyependekezwa na CCM kuwania Ubunge Jimbo la Korogwe mji ambapo sasa atapambana na wapinzania ambapo hata hivyo ameeleza yafuatayo:-.

Katika sekta ya afya 'Obama" anasema amekusudia kutumia mpango wa ushirikishwaji jamii ili kupanga mbinu shirikishi katika kupambana na adui maradhi wilayani humo. Amekusudia kupambana kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hospitali ya wilaya ya Korogwe "Magunga" inapandishwa hadhi na kuwa kama ile ya Tumbi wilayani Kibaha Pwani.

Obama "Yassin" ni mtaalamu wa manunuzi ya kimataifa na masoko ambaye alishawahi kufanya kazi shirika la maendeleo ya petroli TPDC kama mshauri mshawishi wawekezaji. Licha ya hilo "Obama"ni mjasiriamali aliye wekeza katika sekta ya kilimo na ameahidi kushirikiana na Mwalimu wake katika kuwapatia maendeleo wananchi wa wilaya ya Korogwe.

Katika mahojiano na mwandishi wa Makala haya,Obama "Nassir" anasema yeye ni mtoto tu ila ana mbinu na uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Korogwe. "Nashukuru wanaCCM kunipendekeza kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM,la msingi ni mshikamano na ushirikiano...hii ndio mbinu sahihi ya kuwaletea maendeleo"alisema Nassir.

Nassiri ambaye amembwaga kwa mbali Mwalimu wake Joel Bendera anasema anamheshimu baba yake huyo aliyekuwa mwalimu wake kwani anafahamu jiografia ya wilaya hiyo. Kwa upande wa sekta ya afya Nassir anasema anakubali mchango mkubwa wa Naibu Waziri Joel Bendera ambapo akiingia madarakani atahakikisha anayaendeleza mazuri.

"Hebu angalia...'hospitali yetu ya Magunga,inapokea wagonjwa wengi lakini bado haiangaliwi kwa kina,suala la kupandishwa hadhi sio mjadala tena,inabidi tusaidiwe". "Kuna masuala muhimu hapa mfano miundombinu,kuongezewa wataalam wa sekta ya afya kama madaktari bingwa wa mifupa kwani ajali nyingi zinatokea na wanaletwa hapa"alisema.

Nassir anabainisha kuwa la msingi ni suala la utumiaji wa nguvu shirikishi kuiomba wizara ya afya kuboresha miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Korogwe 'Magunga'. Akitanabaisha mazingira ya wilaya ya Korogwe Nassir anasema,mji huo una rasilimali nyingi ambapo kama dhana shirikishi itatumika ipasavyo basi maendeleo yatapatikana.

"Nguvu shirikishi ni tija,nakusudia kuwaletea wanachi fikra,matumaini,na maendeleo zaidi uheshimiwa uweze kukaa sawa katika kuwakomboa wananchi kwenye hali ya unyonge. Anafafanua usemi wake huo kwa kusema heshima ya CCM,wananchi na viongozi wake waliopo madarakani itapatikana iwapo maendeleo yatapatikana Korogwe.

Nassir anasema kwamba siasa ya sasa ni uchumi hivyo kuna kila haja kwa wale wanaopata nafasi kuwashirikisha wananchi katika kujikomboa na hali ya umasikini wa kipato. Hata hivyo Nassir anasema anakusudia kushirikiana na wananchi kuufanya mji wa Korogwe ulioko barabara kuu unaboreka kwa kutafuta wawekezaji watakauwezesha.

"Rasilimali watu na nyingine zilizopo zikitumika ipasavyo uchumi wa wilaya ya Korogwe na watu wake utaimarika, hivyo nasisitiza kwamba nitashirikiana na wananchi wangu".Nassir anaongeza kwamba haoni sababu ya kupanda gari lenye 'tinted' kujificha kwa wananchi ambapo kama mikakati kadhaa haijatekelezeka anakusudia kuwa muwazi kwa yote.

"Kwa nini nipande gari la 'tinted'yote tutakuwa tumepanga pamoja,kama tumefeli tunapeana mrejesho kila siku hivyo dhana hii shirikishi ndio nitakayoitumia"anamaliza. Pamoja na hayo hakusita kuizungumzia sekta ya michezo ambapo alisema atatumia uwezo na uzoefu wa Mwalimu wake Joel Bendera ili wilaya ya Korogwe irudishe hadhi yake.

"Mimi nitashirikiana na Mh.Bendera, anajua kila kitu hapa,ila lazima ieleweke kwamba burudani ni uchumi na ajira hivyo lazima iwepo tija"anabainisha Nassir. Akizungumzia mchakato wa ndani wa chama cha mapinduzi,CCM Nassir anasema umeboreka zaidi na tangu ameingia hajawahi kuona makundi wilayani Korogwe yanayoashiria chuki.

Aidha Nassir anakerekwa na suala la mimba za utotoni kwa wanafunzi suala ambalo kama ataingia kwenye ubunge ameahidi kulifanyia kazi ili liweze kukoma kabisa. Obama (Nassir) anashukuru wale aliyokuwa akipamba nao katika kuwania nafasi ya Ubunge kwa kumpongeza na kumpigia simu ila anasema amekosa mawasiliano na Mwalimu wake.

"Mh.Bendera sina simu yake na nadhani pia yeye hana yangu huyu ndiye hatuwasiliani ila wengine wamekuwa wakinipongeza na tutawasiliana na nakubali ushauri wao". Katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa Korogwe mji Nassir almaarufu 'Obama' alimgaragaza vibaya mwalimu wake Joel Bendera aliyemfundisha shule ya msingi ya Mazoezi Korogwe.

Nassir amezaliwa wilani Korogwe mwaka 1965 ambaye sasa ameingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kupambana na wapinzania kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.


Na Sussan Uhinga, Korogwe.

FIVE BROTHERS YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

WATOTO wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu cha Casa delajoa kilichopo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga wameiomba Jamii kuendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa makundi hayo ili waweze kuishi kwa faraja.

Watoto hao wamesema jukumu la kusaidia yatima ni la kila jamii hivyo wanajamii bado wanahitajika Nkushiriki kuwasaidia ili nao waweze kuishi kama watoto wenye wazazi wao.

Mmoja wa watoto hao Monica Eliasi anayalelewa katika kituo hicho ametoa kauli hiyo leo muda mfupi baada ya kupokea msaada wa Vyakula,Sabuni na Maziwa kutoka kwa Kampuni ya Five Brothers Entertainment.

Awali Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,Bwana Nassoro Makau ameitaka Jamii Mkoani Tanga kujitoa na kuwasaidia watoto yatima kwani kila mwanajamii anajukumu la kufanya hivyo.

Nae Mlezi wa watoto hao Katika Kituo hicho cha Casa delajoa Sista Josephine Sesf ameishukuru Kampuni hiyo na kutoa wito kwa Jamii kuunga mkono juhudi hizo za kuwasaidia watoto hao kwani hao ni Watoto wa Taifa na ni Watoto wa Mungu.

TOUR OPERATORS AND INFORMATION CENTRES IN TANGA!

TANGA

Blue Mango Expeditions
Independence Avenue
Sachak House
P.O. Box 661, Tanga, Tanzania
Phone: +255(0)717032496
+255(0)716919686
E-mail: cindy@expeditions.com
mathias@expeditions.com

*********

Ilya Tours and Safaris
Central Market,
Ocean Breeze Hotel
P.O Box 6128, Tanga, Tanzania
Phone: +255(0)786671163
+255(0)713560569
+255(0)784660569
E-mail: ilyatours@yahoo.com
Website: www.ilyatours.com

********

RH Travels
Domestic Flights Agent
Street No.4 near
Mkwakwani Lodge
Phone: +255(0)653192172
+255(0)272645843
E-mail: rhtravels@hotmail.com

*******

Starword Travels & Tours
Int.&.Dom Flight Agents
Opp. Post Office
Phone: +255(0)272645597
E-mail: starworldtravel_2005@yahoo.com

*******

TAYODEA Tourist Information Center
Market Street,
Opp. NMB Bank, Tanga
Phone: +255(0)272644350
+255(0)713260027
E-mail: tayodea@yahoo.com
Website: www.tayodea.or.tz

LUSHOTO


Friends Of Usambara Society.
Maib Street
Opp. NMB Bank
Phone: +255(0)272640132
+255(0)784420310
E-mail: usambaras2000@hotmail.com

*******

Sed Adventures Tours & Safaris
Opp. NMB Bank
Sun Hotel
Phone: +255(0)784689848
+255(0)754826823
E-mail: info@sedadventures.com
anna@sedadventures.com

*******

TAYODEA Tour Care
Near Bus Stop,
Florida Hotel
Phone: +255(0)272644350
E-mail: youthall2000@yahoo.com
Website: www.tayodea.or.tz

*******

Community Care & Friendship Association
Green Valley Hotel
Phone: +255(0)786861969
E-mail: cocafatz@yahoo.com

*******

KOROGWE

Lutindi Cultural Ecotourism Group
Near Msambiazi Village
13 Km off Main Road
Phone: +255(0)272641040
+255(0)764414491
+255(0)753101618
E-mail: lutindi-hospital@elct.org

*******

PANGANI

Pangani Tourism Information Centre
Phone: +255(0)272630006
Website: www.panganituorism.com

Monday, August 30, 2010

MAKORORA HIYO MZEE!!!

Kanisa maarufu mitaa ya Makorora kwa mbali katika picha huku daladala ya Donge ikipita...barabara hii hupitiwa na daladala zinazofanya safiri za Donge na Sahare. Hapa ni mitaa ya Makorora Tanga.

Njia panda ya kupita daladala za Donge na Sahare.

Msikiti pekee ulipo barabarani eneo la Makorora.

Hapa ni sokoni..hata hivyo kuna shughuli nyengine ambapo wakazi wa Makorora hujipatia mahitaji yao ya kila siku.

Upande mwengine wa eneo la Makorora.

Hapa Ni Tamta Charitable Dispensary..

Makorora pia ni maarufu sana kwa uuzaji wa ndizi.

Soko la Makorora



KALEMBO AWAASA NIDHAMU WAREMBO WA MISS TANZANIA!

Mkuu wa mkoa wa Tanga,Said Kalembo amewataka warembo wanaotarajiwa kushiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania(Miss Tanzania)kuwa na nidhamu wakati wa mashindano hayo.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na warembo hao katika halfa iliyofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa waTanga ikiwa ni ziara ya siku moja ya warembo hao mkoani hapa.

Alisema kuwa kwa sasa kila kitu ambacho kinafanyika na kupata mafanikio makubwa ni lazima liwe nidhamu hivyo kuwataka warembo hao kuzingatia nidhamu wakati wa shindano hilo.

Aidha alisema kuwa warembo hao kwa sasa wana mzigo mkubwa sana na mzigo huo ni kuhakikisha wanashiriki katika shindano hilo wakiwa na nidhamu ya hali ya juu na ni lazima wakubaliane na matokeo ya aina
yoyote yale.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka warembo kuelewa kuwa urembo ni ajira na kazi wala wasikatishwe tamaa na watu wanaosema kuwa ni uhuni kwa sababu uhuni ni hali ya mtu mwenyewe.

Kwa upande wake,Mratibu wa miss Tanzania ,Hashimu Lundenga alisema kuwa wamefarijika na mapokezi hayo na kusema kuwa Tanzania kwa sasa ipo juu sana katika suala la urembo kuliko nchi yoyote ile ya Africa.

Jumla ya warembo 30 wanaotarajiwa kushiriki katika shindano hilo walizuru mkoani hapa na ambapo walipata fuska ya kutembelea vivutio vya mapango ya Amboni(Amboni Calves) yaliyopo mkoani hapa. Katika kinyang'anyiro hicho mkoa wa Tanga unawakilishwa na Jally Murei.

Friday, August 27, 2010

HUYU NDIO SILIKANTI ALIYEVULIWA TANGA!

Samaki mkubwa wa kihistoria duniani ambaye alikuwa amepotea zaidi ya miaka milioni 65 aliibuka katika Kisiwa cha Nyuli, Pwani ya Tanga na kuvuliwa na wavuvi wa eneo la Sahare Jijini hapa.

Samaki huyo aina ya Silikanti amekuwa akipasua vichwa vya wanasayansi ya viumbe wa majini duniani kutokana na umbile lake kuwa na viwiko vya miguu na mikono, pingili na mafuta mengi tofauti na samaki wengine.

Mshauri wa Uvuvi katika Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, Hassan Juma alitoa taarifa hiyo wakati wa kikao cha waandishi wa habari cha kutambulisha shughuli za mradi wa uhifadhi wa mazingira ya baharini na pwani (MACEMP) kwa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.

VODACOM FOUNDATION YAFUTURISHA NA KUTOA MSAADA TANGA!

Wawakilishi wa kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania Vodacom Foundation wakiwa tayari kutoa msaada kwa watoto waishio hapa mkoani Tanga, Pangani kutokea kijiji cha Mwera. Pamoja na kutoa misaada hiyo kampuni ya Vodacom pia iliweza kufuturisha kwenye uwanja Uhuru uliopo pembezeno kabisa na mto Pangani

Mtoto Mohammed Mtoo Ally akipokea msadaa wa Madaftari kutoka kwa mmoja wa mwakilishi wa kampuni ya Vodacom Foundation.

Nae mtoto Bwanga Abdalah akipokea msaada wa Sukari kutoka kwa wawakilishi wa Vodacom waliofika mjini Pangani jana usiku kwa ajili ya kuiwakilisha kampuni yao.

Hawa ni vijana wa Tanesco.....walikuwepo kwa kazi moja tu- pindi umeme ungeleta tafrani basi wangeweka mambo sawa.

VIJIMAMBO VYA TANGA na FULL SHANGWE uso kwa uso....Mimi (Anko Mo) na John Bukuku ambaye pia ni blogger wa full shangwe.

Mashekhe wakifanya utaratibu wa kugawa chakula (Futari) kwa wananchi waliohudhuria uwanja wa Uhuru.

Baada ya kazi ya ugawaji chakula kumalizika, watu ilibidi wakunje goti.

Bismilah!!! futari ilianza kuliwa.

Vijana wakichangamkia futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation.

Thursday, August 26, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!......WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA TANGA!

Wahamiaji haramu kutokea nchi za Ethiopia na Somalia wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi katika kituo kikuu cha wilayani Pangani, punde baada ya kukamatwa. Kulia ni mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Pangani A.S.P Ally Mkalipa.

Wahamiaji hawa alikamatwa kijiji cha Sange, Mkoani hapa baada ya wananchi kutoa taarifa polisi muda mfupi waliposhuka kutoka kwenye jahazi.

"GOMA" NGOMA YA ASILI KUTOKA TANGA

Wednesday, August 25, 2010

MWANAHELA NA KUNDI LA GOLDEN STAR "MKUNA NA MKUNWAJI"

Sikiliza "Mkuna na Mkunwaji" wa Mwanahela akiwa na kundi la Golden Star. Kusikiliza wimbo huo tazama pembeni kulia palipoandikwa TAARAB ZA ZAMANI HAPA!

TANGA CELEBRITIES!!

Ally Mohammed a.k.a Bra A wa Mwambao Fm Radio ya jijini Tanga aliyevaa shati jekundu, anayemfuatia ni Dj Bad Fuvu a.k.a Kichwa Kibovu wa Mwambao Fm pia mwenye fulana nyeupe....Ras Bizzle pamoja na washkaji wengine.

MIHOGO YA KIRARE HIYOOOOO!!

Kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mihogo huuzwa sana.....hapa ni eneo la Kirare nia ya kuelekea Pangani.

Tuesday, August 24, 2010

DEEP SEA- SOKO MAARUFU KWA SAMAKI JIJINI TANGA

Hawa ni baadhi ya samaki wazuri wanaopatikana Deep Sea, moja ya soko linalouza samaki kwa bei nafuu kabisa. Wachuuzi wengi wa samaki jijini Tanga huja hapa na kununua kwa jumla na kisha kusambaza majumbani. Ni eneo la baharini, lipo katikati ya Chumbageni na Kisosora

Samaki wakiwa kwenye meza tayari kwa kuuzwa.

Nilinunua hilo fungu la kwanza kwa ajili ya kitoweo wadau....

Wauzaji wa samaki wakiwa makini katika biashara yao.....hapa alikuwa akizungumza na mteja.

Kwa kipindi hiki cha Ramadhani samaki wamekuwa wakiuzika kwa wingi kutokana na kutumika sana kama kitoweo cha Daku pamoja na Muhogo wa Nazi.

Meza nyengine ikiwa na samaki. Hapa kila dakika samaki huletwa, tena wengine wakiwa bado hai.

Wakazi wa Tanga wakiwa katika harakati za kununua samaki eneo la Deep Sea.

Hii njia inaelekea chini sehemu ambayo kuna bahari na vyombo vya uvuvi wa samaki.

Ukiwa Deep Sea, kuna hii barabara inayoelekea Bandarini. Mizigo mikubwa inayoshuka kwenye meli hupitishwa huku.

Hapa ndio njia panda ya Kisosora Na Chumbageni....kushoto unaelekea Deep Sea na hii nyengine inaelekea Horohoro.

PICHA YA WIKI!!

Mtangazaji wa redio Breeze Fm ya jijini Tanga Benson aliyevaa fulana nyeusi ndani akiwa na Ma'dj wa redio hiyo pia...mwenye shati la kijani ni Dj Roger Kiss pamoka na Dj Bob Nass.

Monday, August 23, 2010

KIVUKO CHA MV PANGANI LEO MCHANA!!

Nahodha wa kivuko cha Mv Pangani akiwa mzigoni leo mchana wakati kivuko hiko kikitoa huduma kwa wananchi wa Pangani.

Kwa mbali kivuko kikijongea upande wa pili wa Pangani kutokea Bweni

Wananchi wakijitaarisha kushuka.

Wakazi wa Pangani wakiteremka kutoka kwenye kivuko hiko kipya cha kisasa zaidi cha Mv Pangani



COASTAL UNION YALETA KOCHA MPYA KUTOKA MOMBASA


KLABU ya Coastal Union yenye maskani yake barabara ya 11 jijini Tanga imesajili kocha mpya kutoka Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo, Ahmed Aurora ameiambia blog hii kuwa tayari kocha huyo ameshawasili jijini hapa tayari kwa ajili ya kuanza kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na ligi daraja la kwanza.

Aurora alimtaja kocha huyo kuwa ni Saidi Ally kutoka Mombasa Kenya na kwamba ataanza rasmi kukinoa kikosi hicho kama kocha mkuu. Alisema kocha huyo awali kabla ya kwenda nchini Kenya alikuwa akiifundisha Klabu ya villa squad ambayo iliweza kupanda daraja kutokana na umahiri wa kocha huyo.

Aliongeza kuwa Kocha huyo na wachezaji 23 wapya waliosajiliwa na klabu hiyo watatambulishwa rasmi kesho( leo jumapili) kwa wanachama wa klabu hiyo katika mkutano wa pamoja utakaofanyika makao makuu ya klabu hiyo barabara ya 11.

Hata hivyo majaliwa ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Mussa Ricco kuendelea kukinoa kikosi hicho bado hayajajulikana


Thursday, August 19, 2010

"HUWEZI JUA"- BWANA MISOSI FT JUA KALI/NEMO

Ngoma mpya ya msanii nguli wa bongo flava kutokea jijini Tanga Bwana Misosi....ngoma inaitwa 'Huwezi Jua' amemshirikisha Jua Kali kutoka nchini Kenya. Imetengenezwa Fish Crab Rec chini ya producer Lamar- Nemo katupiwa katikati kwenye koras!! Kusikiliza wimbo huo tazama hapo juu pembeni palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA CHAMA CHA CUF MKOA WA TANGA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2010


Mussa Mbarouk (Tanga Mjini)

Remmy Shundi (Handeni)

Bakar Mbega (Mkinga)

Abubakar Bakari (Muheza)

Gogola Gogola (Mlalo)

Fabi Sozi (Bumbuli)

Abassy Mkankamghanga (Lushoto)

Jumaa Magogo (Korogwe Mjini)

Mohamed Asiu (Korogwe Vijijini)

Omar Masomaso (Pangani)

WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA CCM MKOA WA TANGA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2010


Tanga mjini: Omari Rashid Nundu

Kilindi: Beatrice Matumbo Shelukindo

Muheza: Herbert James Mntangi

Mkinga: Danstan Luka Kitandula

Pangani: Salehe Ahmed Pamba

Lushoto: Henry Daffa Shekifu

Bumbuli: January Makamba

Korogwe Mjini: Yusuph Nasri

Mlalo:Brig. Gen. Hassan Athuman Ngwilizi

Korogwe Vijijini: Stephen Ngonyani

Handeni: Dr. Abdalah Omari Kigoda


Wednesday, August 18, 2010

UJUMBE WA ROMA AKIWA NJIANI KUJA TANGA LEO!

"Nipo in raha leo bus...naelekea tanga nyumbani...4 holiday...na piiia nitapata muda mzuri sn wa kuchora lyrics...na v2 kaa hzo....sasa nitakaporudi dar sasa...eee jombaa inabidi wajipaaangeee...coz nimesafiri na dozen ya beatz za j.ryder....asalam aleykum tanzania....ki2 cha mbezi tym hzi naitafuta mlandizi....ilalee jombaa" kutoka facebook yake!!

MZIGO UMEINGIA....!

Umependa fulana ama kapelo..? Wasiliana na mimi nikupatie kwa bei nafuu kabisa.

Kitu cha white...

Kitu cha kofia...

Kitu cha green..

Wasiliana na mimi mapema ili uwe mjanja katika kuutangaza mkoa wetu wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.