BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, June 13, 2009

MWAMBAO FM ILIVYOVUMBUA VIPAJI VYA UWIMBAJI!!


Dj Shago 66 na Dj Bob Nas wa Mwambao Fm wakiweka mambo sawa kuhakikisha muziki unatoka vizuri ili kuwapa shangwe mashabiki pamoja na wasanii.


Msanii kutoka kundi la Street Coulor akiwakilisha vya kutosha kwenye stage. Fainali hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite.

Star B akiwa kama ni solo artist, akijituma ipasavyo kuhakikisha anaibuka bingwa!


Masotojo kutoka Tanga alipiga show katika harakati za kuchuja wasanii watakaoingia mkataba na Mwambao Fm kupitia Mwambao Record.


Mshiriki anayejulikana kwa jina la The Drama, akionyesha kipaji chake jukwaani.

Wazee wa Shino Style- Shomy Luv pamoja na Big Smart wakitoa burudani kali kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite siku hiyo ambapo wasanii wanne waliweza kuingia mkataba na Mwambao Record.


Baadhi wa Presenters wa Mwambao Fm, Mamaa Nusura Abdalah wa kwanza- Dj Rach Kuty aliyevaa fulana ya kijani pamoja na Benedict Kaguo a.k.a Father K wakifuatailia kwa makini fainali hiyo.


Usipiime!! Kulijaa watu sio mchezo. Hakuna aliyetaka kupitwa- wadau wote wa muziki wa bongo flava waklikutana hapa.



Majaji walikuwa na kazi nzito!! Wa kwanza ni Jaji Anko Mo kutoka Mwambao Fm na aliyevaa kofia ni Dr Leader ambaye pia ni msanii- pamoja na Sam Chad Producer kutoka King Falcon.


Dr Leader na Sam Chad wakiteta jambo.

Leader akaona haitoshi- akamgeukia Anko Mo kwa kuteta mengine zaidi.


Dj Bob Nas akijaribu kumueleza jambo mshereheshaji wa fainali hiyo Ahmed Khatibu (wawoo)- Shindano hilo la kutafuta vipaji lilidhaminiwa na redio Mwambao Fm kwa lengo la kuwapa vijana ajira kupitia tasnia ya muziki. Washindi walikuwa ni Razy Flava, Chabo, Star B pamoja na The Drama.


No comments:

Post a Comment