BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, June 9, 2009

GLORY CHUWA AIBUKA MSHINDI MISS TANGA 2009


MREMBO Glory Chuwa(20) ameibuka kuwaMiss Tanga Vodacom 2009 baada ya kuchaguliwa na jopo la majaji kuwamshindi katika mchuano mkali uliofanyika usiku wa jumamosi kwenyeuwanja wa Mkwakwani Jijini hapa.


Glory ambaye ametokea kitongojicha Miss College, alifanikiwa kupita katika chekeche la mchujouliowashirikisha warembo 20 waliokuwa wameshinda kwenye vitongoji vyaWilaya za Mkoa wa Tanga na kuingia kambi ya Miss Tanga kwa kipindi chawiki tatu.


Baada ya Mkurugenzi wa Five Brothers Enterteinment,Nassa Makau, kumtaja Glory kuwa ndiye mshindi,mrembo huyo alivikwarasmi taji na Miss Tanga 2008,Nadia Ahmed na amezawadiwa sh. 1 milioni.

Jopo hilo la majaji likongozwa na aliyewahi kuwa Mr College nchini MatukioChuma,lilimchagua Yasmin Zachari kuwa mshindi na miss Tanga namba tatuni Rachel Mlaki,wakati aliyeshika namba nne Alice Marcus na kufuiatiwana Neema Mbuya.

Shindano hilo liliandaliwa na Five Brothers Entertainment ikishirikiana na wadau wengine- Natumai dada yetu Glory Chuwa utatuwakilisha vyema mkoa wetu wa Tanga huko uwendapo. Ila nakuomba sana kwepa skendo!!


No comments:

Post a Comment